Kagera (mto)
From Wikipedia
Mto wa Kagera (Kinyarwanda: Akagera) ni kati ya mito inayounda mto wa Nile pia ni mto mkubwa kabisa wa kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.
Inaanza Burundi inapounganika mito ya Nyawarongo (Niavarongo) na Ruvubu (Ruvuvu) ikiendela 400 km hadi kuingia ziwa la Viktoria Nyanza.
Mto wa Kagera ukielekea kaskazini ni mpaka kati ya Tanzania na Rwanda; pale inapogeuka kuelekea mashariki karibu na mji wa Kikagati ni mpaka kati ya Tanzania na Uganda. Sehemu ya mwisho wa njia yake inaingia kabisa ndani ya eneo la Tanzania hadi kufika Viktoria Nyanza kama 40 km kaskazini za Bukoba.
Jina la mto wa Kagera umekuwa pia jina la mbuga ya wanyama ya Akagera National Park huko Rwanda na pia la Mkoa wa Kagera katika Tanzania.