Kwando
From Wikipedia
Mto wa Kwando (Cuando) | |
---|---|
|
|
Chanzo | Nyanda za juu za Bié (Angola) |
Mdomo | Mto Zambezi kwa mji wa Kazungula (Zambia) |
Nchi | Angola, Zambia, Namibia, Botswana |
Urefu | 1,500 km |
Kimo cha chanzo | 1,700 m takriban |
Mkondo | ?? |
Eneo la beseni | 96,778 km² |
Kwando (au: Cuando; kabla ya mdomo pia Linyanti halafu Chobe) ni mto wa Afrika ya Kusini na tawimto wa Zambezi. Chanzo chake iko nyanda za juu za Bié (Angola) inapoelekea kusini-mashariki. Inakuwa mpaka kati ya Angola na Zambia kwa 140 km halafu inapita Kishoroba cha Caprivi na kuwa mpaka kati ya Namibia na Botswana.
Inaingia katika mabwawa wa Linyanti yenye 1,425 km². Katika sehemu hizi mto huitwa kwa majina Chobe au Liyanti.
Kwa jina la Chobe unaingia katika mto Zambezi kwenye mji wa Kazungula pale ambako nchi nne za Botswana, Namibia, Zambia na Zimbabwe zinakutana.