Leo Esaki
From Wikipedia
Leo Esaki (amezaliwa 12 Machi, 1925) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Reiona Esaki. Hasa alifanya utafiti upande wa ufundi mitambo wa kwanta. Mwaka wa 1973, pamoja na Ivar Giaever na Brian Josephson alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.