Matatu
From Wikipedia
Matatu ni neno la kawaida nchini Kenya la kutaja gari aina la minibus linalotumika kama usafiri wa umma. Jina la "matatu" hutokea na nauli ya shilingi tatu iliyokuwa kawaida kwa safari moja matatu zilipoanza.
Mara nyingi ni magari ya Kijapan yenye ruhsa ya kubeba abiria 14. Matatu huhudumia njia maalumu yenye namba yake. Dereva anafanya kazi yake pamoja na msaidizi wake anayeitwa "manamba" mwenye kazi ya kukusanya pesa na kufungua au kufunga mlango.
Hadi mwaka 2003 matatu hayakufuata utaratibu huu wala taratibu nyingine. Ilikuwa kawaida kuingiza zaidi ya watu 20 katika gari moja lenye viti 20. Maafisa wa polisi ya barabarani (traffik) yalizoea kupokea hogo za matatu kila siku hivyo walishindwa kuwaambia neno.
Serikali mpya ya Rais Mwai Kibaki iliweza kubadilisha hali hiyo hasa waziri wa usafiri John Michuki aliyelazimisha wenye matatu kukubali utaratibu ambao haukuwa mpya lakini ulipuuzwa miaka mingi hadi kusahauliwa isipokuwa wazee walikumbuka siku za kale.
Tangu mwanzo wa 2004 matatu yanatakiwa kuonyesha nje kanda ya rangi ya njano; dereva na manamba wawe na sare, kila kiti kinapaswa kuwa na kanda, na matatu kama mabasi yanatakiwa kuwa na "gavana" yaani chombo cha kukata mkasi wa gari likipita 80 km/h.
Utaratibu huu umeanza kuvurugika tena lakini bado hali ni afadhali kuliko zamani hasa idadi ya vifo imepungua.