Mbabane
From Wikipedia
Mbabane ni mji mkuu wa Uswazi ikiwa na wakazi 70,000 (2003). Ofisi za serikali ziko hapa lakini bunge na jumba la mfalme ziko mjini Lobamba.
Mji uko kwenye milima ya Mdimba kwenye kimo cha 1200m juu ya UB.
[edit] Historia
Mji ulianzishwa na Waingereza mwaka 1902 BK baada ya vita dhidi ya makaburu ukawa makao makuu ya kiutawala wa eneo la Uswazi. Jina limetokana na chifu Mbabane Kunene aliyekuwa mkuu wa sehemu ile wakati wa kuunda mji.
[edit] Uchumi
Nguvu ya kiuchumi ya Mbabane ni migodi ya karibu ya bati na dhahabu.