Moroni (Komori)
From Wikipedia
Moroni (Mwandiko wa Kiarabu: موروني) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Komori mwenye wakazi 60,200.
Mji uko upande wa magharibi wa kisiwa cha Ngazija (Grande Comore). Kuna bandari kwa usafiri kwa meli kwenda visiwa vingine vya bahari Hindi pia bara la Afrika ya Mashariki pamoja na uwanja wa kimataifa wa ndege.
Anwani ya kijiografia ni 11°45′S 43°12′E.
[edit] Historia
Moroni ilikuwa mji mkuu wa Usultani wa Bambao uliokuwa dola lenye kipaumbele kisiwani hadi kuja kwa ukoloni wa Ufaransa.