Pearl S. Buck
From Wikipedia
Pearl Buck (26 Juni, 1892 – 6 Machi, 1973) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Marekani. Jina lake la kuzaliwa ni Pearl Comfort Sydenstricker; Buck ni jina la mume wake. Lakini aliandika chini ya jina la John Sedges. Anajulikana hasa kwa riwaya zake juu ya maisha katika nchi ya Uchina ambapo alilelewa akiwa mtoto wa wamisionari. Mwaka wa 1938 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.