Roma
From Wikipedia
Roma (pia: Rumi) ni jina la mji wa Roma (mji mkuu wa Italia) ama jina la dola la Roma lililokuwa dola kubwa zamani.
[edit] Roma au Rumi?
Roma ni umbo la jina katika Kilatini na Kiitalia; imekuwa kawaida katika Kiswahili cha kisasa. "Rumi" ilikuwa kawaida katika Kiswahili cha zamani kutokana na kawaida ya lugha ya Kiarabu (الرُّومُ ar-Rūm). Matoleo ya Biblia ya "Union Version" iliyochapishwa tangu 1952 hutumia "Rumi", "Warumi". Tafsiri ya Biblia ya Kiswahili cha Kisasa hutumia "Roma", "Waroma".
- Mji wa Roma, jina la mji mkuu wa nchi ya Italia
- Dola la Roma, dola kubwa katika eneo la Mediteraneo (Ulaya, Asia ya Magharibi, Afrika ya Kaskazini) mnamo miaka 2100-1600 iliyopita. Limeendelea katika Dola ya Roma ya Mashariki au Bizanti hadi mwaka 1453 b.K.
- Roma ilikuwa jina la mungu wa kike katika dini ya Roma ya Kale
- Miji mingine inayoitwa kwa jina la "Roma" iko Australia, Ecuador na Marekani; pia eneo ndani ya mji wa Mexiko.
- Kutokana na jina la mji yamepatikana majina ya:
- Roma, meli ya kijeshi ya Italia;
- Roma ni jina la filamu mbalimbali;
- Roma ya Kale