Rombo
From Wikipedia
Rombo ni miongoni mwa wilaya sita za mkoa wa Kilimanjaro upande wa mashariki ya mlima. Mkuu ni makao makuu ya wilaya hiyo. Warombo ni sehemu ya Wachagga.
Wilaya imepakana na Kenya upande wa kaskazini na mashariki, wilaya ya Hai upande wa magharibi na wilaya ya Moshi vijijini upande wa Kusini.
Idadi ya wakzi ni 246,479 (sensa ya 2002) [1].
[edit] Tarafa
Kuna tarafa 20 zifuatazo:
- Katangara Mrere
- Kelamfua Mokala
- Keni Aleni
- Keni Mengeni
- Kirongo Samanga
- Kirwa Keni
- Kitirima Kingachi
- Mahida Holili
- Makiidi
- Mamsera
- Mengwe Manda
- Motamburu Kitendeni
- Mrao Keryo
- Nanjala Reha
- Olele
- Shimbi
- Tarakea Motamburu
- Ubetu Kahe
- Ushiri Ikuini