Saint-Denis (Reunion)
From Wikipedia
Saint-Denis (au Saint-Denis de la Réunion) ni mji mkuu wa eneo la ng’ambo la Ufaransa (yajulikana kwa Kifaransa kama "département d'outre-mer") la Réunion ambayo ni kisiwa kimoja cha funguvisiwa ya Maskarena katika Bahari Hindi.
Saint-Denis ni pia mji mkubwa wa kisiwa ikiwa na wakazi 131,557 (mwaka 1999).
[edit] Historia
Saint-Denis ilianzishwa na Mfaransa Étienne Régnault mnamo mwaka 1669 ikawa mji mkuu wa kisiwa mwaka 1738.
[edit] Usafiri
Kuna kiwanja cha ndege cha Aéroport de la Réunion Roland Garros ambayo ni geti ya kisiwa kwa safari za kimatifa. Bandari kuu ya kisiwa iko Pointe-des-Galets nje ya mji.
[edit] Viungo vya nje
- Ukurasa rasmi wa mji (Kifaransa)