Tadeus Reichstein
From Wikipedia
Tadeus Reichstein (20 Julai, 1897 – 1 Agosti, 1996) alikuwa mwanakemia kutoka nchi ya Uswisi, lakini alizaliwa Poland. Hasa alichunguza homoni katika gamba la tezi adrenali. Mwaka wa 1950, pamoja na Edward Kendall na Philip Hench alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.