Tana (mto)
From Wikipedia
Tana ni mto mrefu wa Kenya ukiwa na urefu wa takriban 650 km. Chanzo chake ni milima ya Aberdare magharibi ya Nyeri. Mwanzoni inelekea mashariki halafu ina pinde kuzunguka Mlima Kenya upande wa kusini, kuelekea tena kaskazini na kuwa na pinde tena kuelekea sasa Bahari Hindi kwa mwendo wa kusini-mashariki.
Inapita miji ya Garissa, Hola na Garsen kabla ya kufika Bahari Hindi kwenye Ghuba ya Ungwana.