Tukuyu
From Wikipedia
Tukuyu ni mji mdogo na makao makuu ya wilaya ya Rungwe katika mkoa wa Mbeya, Tanzania. Iko kwa 1300 m juu ya UB karibu na mlima wa Rungwe ikitazama beseni ya Ziwa Nyasa.
Contents |
[edit] Historia
Tukuyu ilianzishwa wakati wa ukoloni wa Kijerumani ikaitwa Neu Langenburg ("boma ndefu mpya") badala ya Langenburg ya awali iliyokaa mwambaoni wa Ziwa Nyasa ikazama chini wakati wa maji ya ziwa kupanda. Hadi leo jina la hoteli "Langiboss" inakumbuka jina la zamani. Neu Langenburg ilikuwa mji mkuu wa mkoa wa kusini (takriban mkoa wa Mbeya wa leo). Wakati wa Waingereza ikapewa jina la Tukuyu ikawa mji mkuu wa wilaya.
[edit] Uchumi
Tukuyu iko katika eneo penye mvua nyingi na rutba; ni kitovu cha kilimo cha chai Tanzania.
Tukuyu ilikuwa miaka mingi na tatizo la mawasiliano mabaya kutokana na uharibifu wa barabara pamoja na matatizo ya kisiasa kati ya Malawi na Tanzania. Siku hizi Barabara ni nzuri kuelekea Malawi pia kwenda Mbeya na Daressalaam. Kuna nafasi nzuri ya utalii kwa sababu ya uzuri wa mazingira. Lakini huduma bado ni chache.
[edit] Wakazi
Tukuyu ni eneo la Konde au Wanyakyusa. Mji mwenyewe umekuwa kituo cha daiyosisi ya Konde ya Waluteri pia daiyosisi ya Wakatoliki. Makao makuu ya Moravian bado yako Rungwe misioni.
[edit] Taasisi
Tukuyu ina shule za sekondari, Chuo cha Ualimu na taasisi ya utafiti wa tiba. Kuna pia ofisi za serikali au umma vya wilaya, Posta, simu, hospitali ndogo, benki.