Ufalme wa Kongo
From Wikipedia
Ufalme wa Kongo ulikuwa dola la Afrika ya Kati. Eneo lake lilikuwa ndani ya nchi za leo Kongo (Kinshasa), Angola na Kongo (Brazzaville).
Ulianzishwa katika karne ya 14 ikadumu hadi karne ya 17. Mtawala wake alikuwa na cheo cha "Mwene Kongo" au "Manikongo" wa kabila la Bakongo.
Ufalme huu umejulikana zaidi kihistoria kwa sababu ya mawasiliano yake ya kimataifa. Katika karne ya 15 meli za Wareno zilifika mwambanoni mwake. Manikongo mbalimbali zilijenga uhusiano na Ureno na Kongo ilikuwa taifa la kushikamana na Ureno hadi kuharibika kwa uhusiano huo. Katika kipindi kile taarifa mbalimbali ziliandikwa zinazotupa leo picha nzuri ya ufalme huo.
[edit] Jiografia
Wakati wa kukutana na Wareno Ufalme wa Kongo ulikuwa na eneo la labda 300,000 km² ukaunganisha robo ya magharibi ya Kongo (Kinshasa) pamoja na sehemu za Angola na Kongo (Brazzaville).
[edit] Utawala
Ufalme ukawa na majimbo, wilaya na vijiji. Majimbo yalikuwa saba ya Mpemba, Nsundi, Mpangu, Mbata, Mbamba na Soyo. Kwa mikataba ya baadaye falme za Kakongo, Loango na Ngoy likatokea shirikisho ya sehemu nne.