Willy Puchner
From Wikipedia
Willy Puchner ni mu Austria, alizaliwa tarehe 15 March 1952. Puchner ni Mpiga picha, Msanii, Mchoraji na Mtunzi
Contents |
[edit] Historia yake
Puchner alizaliwa na kukulia Mistelbach an der Zaya, Lower Austria, ambako wazazi wake walikuwa na studio ya kupigia picha. Mnamo mwaka 1967 alihamia Vienna alikokwenda kujifunza upigaji wa picha katika Taasisi ya Utafiti na Mafunzo ya Shirikisho la Vienna cha sanaa ya picha. Baada ya kuhitimu mwaka 1974, alifanya kazi ya ukufunzi katika chuo hicho kwa miaka miwili. Kuanzia mwaka 1978, Puchner alifanya kazi kama mpiga picha na mwandishi wa kujitegemea akiwa na makazi yake jijini Vienna. Hadi mwaka mwaka 1983 alipoanza mafunzo ya Filosofia, Historia na Elimu ya jamii.
Puchner alihitimu mafunzo hayo na kupata Shahada ya Uzamili katika somo la Filosofia mnamo mwaka 1988. Andiko lake (Thesis) aliliita "Über private Fotografie") (Upigaji picha wa Kujitegemea). Kuanzia mwaka 1988 ametoa mihadhara mbali mbali juu ya "Upigaji picha wa Kujitegemea" katika Vyuo vikuu, Nyumba za makumbusho na Vituo vya maonyesho. Kuanzia mwaka 1989 Puchner amekuwa akifanya kazi mara kwa mara na hufanya kazi na gazeti la "Wiener Zeitung", (gazeti la zamani la kila siku kuliko gazeti lolote duniani).
Vile vile, Willy Puchner hupendelea kufanya kazi na watu wenye umri mkubwa na alianzisha miradi kama "Die 90 jährigen" (Katika umri wa miaka 90), "Dialog mit dem Alter" (Jadiliana na watu wenye umri mkubwa), "Die 100-jährigen" (Katika umri wa miaka 100), "Lebensgeschichte und Fotografie" (Historia ya mdomoni na Picha) na "Liebe im Alter" (Mapenzi katika umri mkubwa).
[edit] Maonyesho
- Museum Moderner Kunst (Museum of Modern Art), Vienna (Austria)
- Künstlerhaus (House of Artists), N.Ö. Galerie, Vienna (Austria)
- Museum des 20. Jahrhundert (Museum of the 20th Century), Vienna (Austria)
- Steirischer Herbst, Graz
- Berlin, Bremen, Kleve, Braunschweig (Ujerumani)
- Norfolk, Washington, (Marekani)
- Bombay (India)
- Beirut (Lebanon)
- Tokyo, Osaka, Oita, Nagoya, Sapporo (Ujapani)
[edit] Machapisho
Extrablatt, konkret, Stern, Geo, Life, Mare, Corriere della Sera, Marco Polo, Universum, Falter, Wiener Zeitung
[edit] Maandiko ya historia ya maisha
- Bäume, 1980, (Text Henry David Thoreau), ISBN 3-85447-271-4
- Zum Abschied, zur Wiederkehr, 1981 (Text Hermann Hesse), ISBN 3-20601-222-8
- Gestaltung mit Licht, Form und Farbe, 1981, ISBN 3-87467-207-7
- Strahlender Untergang, (Text Christoph Ransmayr), 1982, ISBN 3-85447-006-1
- Andalusien, 1983, ISBN 3-7658-0420-7
- Die Wolken der Wüste, 1983 (mit einem Text von Manfred Pichler), ISBN 3-89416-150-7
- Dorf-Bilder, 1983, ISBN 3-21800-387-3
- Zugvögel seit jeher, 1983, (Text Erich Hackl), ISBN 3-21024-848-6
- Das Herz des Himmels, 1985, (Text Erich Hackl), ISBN 3-21024-813-3
- Die Sehnsucht der Pinguine, 1992, ISBN 3-44617-200-9
- Ich bin ..., 1997, ISBN 3-79182-910-6
- Tagebuch der Natur, 2001, ISBN 3-85326-244-9
- Flughafen. Eine eigene Welt, 2003, ISBN 3-85326-277-5
- Illustriertes Fernweh. Vom Reisen und nach Hause kommen, 2006,.ISBN 3-89405-389-5