Alice Lakwena
From Wikipedia
Alice Lakwena, pia: Alice Auma (1956 - 17 Januari 2007) alikuwa kiongozi wa kiroho kati ya Waacholi wa Uganda aliyeanzisha kundi la "Harakati ya Roho Mtakatifu" (Holy Spirit Movement) na kuendesha vita ya msituni dhidi ya serikali ya rais Yoweri Museveni kuanzia Agosti 1986 hadi November 1987.
Alizaliwa kwa jina la Alice Auma. Baada ya ndoa mbili zilizotengwa alikuwa Mkatoliki. Tar. 25 Mei 1985 alishikwa na mapepo akaonekana kama kichaa. Baada ya kupotea kwa siku 40 akarudi kama mganga wa kienyeji akiwa na kipaji cha kuwasiliana na mizimu kufuatana na utamaduni wa Kiacholi.
Pepo aliyesema mara nyingi kutoka kwake akajiita "Lakwena" na kutambulishwa kuwa roho ya afisa wa kijeshi wa Italia.
Wakati wa kipindi cha vita ya wenyewe kwa wenyewe wa 1986 nchini Uganda Alice alitangaza kwamba aliambiwa na Lakwena kuanzisha Harakati ya Roho Mtakatifu na kuwaita Waacholi wachukue silaha kumaliza vita na umwagaji wa damu. Wamisionari katika eneo walipewa barua iliyosema:
-
- "Mungu Bwana aliyemtuma Lakwena aliamua kubadilisha kazi yake kutoka mganga kuwa kiongozi wa kijeshi. Haina maana kumpona mtu leo akiuawa kesho. Hivyo Lakwena hana budi kumaliza umwagaji wa damu kwanza kabla ya kuendelea kama mganga."
Akapata wafuasi na kushambulia jeshi la serikali akashinda mara kadhaa na kuwaongoza wafuasi wake kuelekea Kampala. Akawaambia waumini kwamba risasi hazitawaudhi zitageujia kuwa maji tu. Baada ya kushindwa kabla ya kufika mji mkuu Lakwena akaondoka kutoka katika Alice. Alice akakimbia Kenya akakaa katika kambi la wakimbizi la Daadab.
Mdogo wake Joseph Kony alikusanya baadaye mabaki ya kikosi chake na kuunda kundi jipya la "Lord's Resistance Army".
Alice alikufa huko Daadab tar. 17 Januari 2007 kutokana na ugonjwa usioeleweka.