Joseph Kony
From Wikipedia
Joseph Kony (* mnamo 1961) ni Mwuganda kutoka Acholi na mkuu wa jeshi la Lord's Resistance Army (LRA = Jeshi la Upinzani la Bwana) ambali ni kikundi cha wanamigambo wa porini ambacho kimepigania vita dhidi ya serikali hadi 2006 kwa kuua watu wengi katika kaskazini ya Uganda na kuteka nyara watoto maelfu waliolazimihswa kuwa askari zake.
Contents |
[edit] Asili za Kony
Kony alizaliwa katika kijiji cha Odek karibu na Gulu katika Acholi. Alibatizwa kuwa Mkatoliki hakumaliza shule.
Alimfuata shangazi yake Alice Lakwena katika vita ya Harakati ya Roho Mtakatifu. Baada ya kushindwa kwa Alice na mwisho wa jeshi lake Kony aliendelea kungoza kundi ndogo ya askari waliobaki pamoja.
[edit] Sauti za mapepo
Kony alidai kuwa alipokea sauti za mapepo pamoja na Roho Mtakatifu waliomwambia kuendelea na vita. Kony alidai ya kwamba shabaha ya vita ni kuanzisha utawala wa Mungu chini ya Amri Kumi za Biblia.
[edit] Mchanganyiko ya dini
Wakimbizi waliofaulu kutoka katika makambi yake wamesema ya kwamba anatumia mchanganyiko wa dini mbalimbali:
- siku za Jumamosi alisali kwa namna ya kikristo na kutumia tasbihi kama Wakatoliki
- siku za Ijumaa alisali sala ya Al-Jummaa ya Waislamu
- alisheherekea Krismasi
- alifunga saumu wakati wa Ramadhani
- alikataza kula nyama ya nguruwe
- sadaka kwa mapepo zilitolewa kwa namna ya Kiacholi
- aliwaruhusu wanaume kuwa na wake wengi akawa mwenyewe na idadi kubwa ya wake
[edit] Vita za Kony
Kati ya 1987 - 1994 Kony aliendesha vita yake katika sehemu za Acholi katika kaskazini ya Uganda. Tangu 1994 alihamia Sudan ya Kusini kwa sababu ya mashambulio makali zaidi dhidi yake na jeshi al Uganda. Alijenga makambi kati Sudan -wengi wanasema alipata usaidizi wa serikali ya Sudan iliyochukizwa na msaada wa Kampala kwa ajili ya SPLA- na kushambulia ndani ya Uganda. Wakati ule askari zake walianza kulipiza kisasi kwa Waacholi waliodhaniwa kuwa walishirikiana na serikali kwa kuwaua au kukata mikono, masikio, miguu au midomo ya watu.
Tangu 1994 aliamuru pia kutekwa nyara kwa watoto na vijana waliolazimishwa kutembea hadi Sudan; wavulana waliingizwa katika jeshi lake na wasichana walichukuliwa kama "wake" wa askari zake; Kony anasemekana alipenda kuchagua kati ya mabinti hawa.
Mwaka 2002 jeshi la Uganda ilipatana na Sudan ikapata kibali cha kushambulia makambi ya Kony ndani ya Sudan. Jibu la Kony ilikuwa kurudi Uganda na kuwaua watu wengi zaidi kuliko awali lakini jeshi la Uganda iliongeza pia askari zake.
[edit] Mashtaka mbele ya Mahakama Kuu ya Kimataifa
2003 Kony pamoja na viongozi wenzake walishtakiwa mbele ya Mahakama Kuu ya Kimataifa kwa hatia za
- jinai dhidi ya ubinadamu na mauaji
- jinai ya kuteka watumwa
- jinai ya ubakaji
- matendo ya kinyama ya kuumiza watu (kukata viungo vya mwili)
- kuumiza watu raia (wasio wanajeshi) kwa kusudi
- kuwalazimisha watoto wadogo kuwa wanajeshi
Mwaka 2005 LRA ililazimishwa kuhamisha kambi lake ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lakini iliendelea kushambulia sehme zu Uganda ya Kaskazini.
[edit] Majadiliano ya 2006 juu ya amani
Mwaka 2006 Kony alimruhusu makamu wake Vincent Otti kuanzisha majadiliano na serikali ya Yoweri Museveni. Majadiliano yalifanyika mjini Juba katika Sudan.
Kony na viongozi wenzake waliahidi ya kwamba watamaliza vita na kuwaruhusu askari warudi kwao wasipokamatwa na kupelekwa mahakamani. Agosti 2006 LRA ilitangaza kusimamisha vita.
Kati Septemba 2006 vikosi ya LRA vilianza kurudi Uganda na kukutana na wanajeshi wa serikali waliowaongoza kuelekea makambi.
[edit] Viungo vya Nje
- About The Acholi People
- Acholi Community Web Portal
- I want peace, but Museveni is the problem, says Kony , transcript of Joseph Kony's call in to a political talk show on the Mega FM radio station broadcasting from Gulu on 28 December 2002
- Kony's eldest son killed, New Vision, 8 July 2005
- Profile: Ugandan rebel Joseph Kony, BBC News, last updated 7 October 2005
- J. Carter Johnson, Deliver Us from Kony, Christianity Today, January 2006
- Portrait of Uganda's rebel prophet, painted by wives, Mail & Guardian, 10 February 2006
- Sam Farmar, Uganda rebel leader breaks silence (interview with downloadable audio in MP3 format), BBC Newsnight, 28 June 2006
- Ruud Elmendorp, Joseph Kony gives press conference (video report from Joseph Kony in his outpost in the Congo), Ruud Elmendorp, 2 August 2006
- Ruud Elmendorp's video interview with Joseph Kony on Rocketboom 16 August 2006
- Ochola John, LRA victim: 'I cannot forget and forgive', BBC, 29 June 2006