Arthur Schawlow
From Wikipedia
Arthur Leonard Schawlow (5 Mei, 1921 – 28 Aprili, 1999) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Kama mtoto na kijana aliishi na kusoma nchini Kanada kabla hajarudi Marekani. Hasa alichunguza mnururisho na kubuni leza alipofanya kazi pamoja na Charles Townes. Mwaka wa 1981, pamoja na Nicolaas Bloembergen na Kai Siegbahn alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.