Atolli
From Wikipedia
Atolli ni kisiwa ambacho ni vipya vya matumbawe inyaoonekana juu ya uso wa bahari. Mara nyingi umbo ni kama mviringo na kuna bwawa la maji katikati. Pia ukingo huu wa matumbawe umevunjika mara nyingi hivyo inaonekana kama mwviringo wa visiwa vidogo na vyembamba.
Karibu atolli zote za dunia ziko katika Pasifiki na katika Bahari Hindi. Atlantiki ina atolli chache katika bahari ya Karibi.
Contents |
[edit] Jina
Neno atolli limetokana na lugha ya wenyeji wa Maldivi "atholhu". Limepokelewa katika lugha ya Kiingereza likajulikana hasa kutokana na maandiko ya Charles Darwin aliyeeleza visiwa hivi kwa upana pamoja na nadhari ji9nsi zinavyokua.
[edit] Asili na kukua kwa atolli
Asili ya atolii huwa ni kisiwa cha volkeni kilichozama chini ya maji. Matumbawe yaliyokua kando la kisiwa hiki yanaendelea kustawi kama kisiwa kinazama polepole sana. Hivyo atolli inaendelea kama mkasi wa kukua kwa matumbawe unalingana na mwendo wa kuzama kwa kisiwa chenyewe.
Kuna mifano ya atolli ambako kelele cha mlima wa katika bado inaonekana.
[edit] Atolli hatarini
Atolli nyingi za dunia ziko hatarini ya kupotea kutokana na kupanda kwa uwiano wa bahari.
[edit] Mifano
|
|
||
|
|
|
![]() |
Makala hiyo kuhusu "Atolli" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Atolli kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |