Nauru
From Wikipedia
|
|||||
Wito la taifa: "God's Will First" | |||||
Wimbo wa taifa: Nauru Bwiema | |||||
Mji mkuu | (hakuna) 1 |
||||
Mji mkubwa nchini | Yaren | ||||
Lugha rasmi | Kiingereza , Kinauru | ||||
Serikali
Rais
|
Jamhuri Ludwig Scotty |
||||
Uhuru kutoka ulinzi wa Australia, New Zealand, na Uingereza -kwa niaba ya UM |
31 Januari 1968 |
||||
Eneo - Jumla - Maji (%) |
21 km² (ya 227) ‘‘(kidogo sana)’’ |
||||
Idadi ya watu - Julai 2005 kadirio - Msongamano wa watu |
13,005 (ya 220) 621/km² (ya 13) |
||||
Fedha | Dollar ya Australia (AUD ) |
||||
Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
(UTC+12) (UTC) |
||||
Intaneti TLD | .nr | ||||
Kodi ya simu | +674 |
Nauru ni nchi ya kisiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya kusini. Ni nchi ndogo sana yenye 21 km² pekee na wakazi 13,000.
Kisiwa jirani ya karibu ni Banaba katika Kiribati chenye umbali wa 300 km. Nauri haina mji mkuu.
Nauru imekaliwa na mchanganyiko wa watu kutoka Polynesia na Mikronesia tangu karne nyingi. Katika karne ya 19 kisiwa kilitwaliwa na Ujerumani kama sehemu ya koloni zake za Pasifiki. Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia kilikuwa eneo lindwa chini ya UM na utawala ulikuwa mkonono wa nchi tatu za Australia, New Zealand na Uingereza. Uhuru ulipatikana tagu 1968.
Uchumi wa Nauri ulitegemea fosfeti iliyopatikana kisiwani kwa wingi. Kwa miaka kadhaa kisiwa kilikuwa nchi tajiri kabisa. Hadi 2001 huduma za hospitali zilikuwa bure, hapakuwa na kodi na watu wengi walikuwa na magari mawili au matatu. Tangu kumaliza kwa fosfeti hali ya kiuchumi imekuwa vigumu sana. Serikali haina pesa tena na huduma nyingi zimekwama. 90 za wananchi wanakosa kazi.
Serikali imeanza kupokea msaada kutoka Australia.
Makala hiyo kuhusu "Nauru" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Nauru kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Nauru