Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
From Wikipedia
Bendera ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imepatikana tangu Februari 2006 kutokana na katiba mpya ya nchi. Katiba iliazimia kurudi kwa mfano wa bendera iliyowahi kutumiwa kati ya 1963 na 1971 kabla ya nchi haijaitwa "Zaire". Buluu yake imebadilishwa kuwa buluu ya angani sawa na bendera ya uhuru ya mwaka 1960.
Buluu ya bendera inakatwa na mlia wa hanamu mwenye rangi za nyekundu na dhahabu. Nyekundu ilimaanisha damu ya mateso chini ya ukoloni na mapabano kwa ajili ya uhuru. Dhahabu ilikumbusha juu ya utajiri wa nchi. Nyota ya rangi dhahabu iko kwenye pembe la juu jinsi ilivyokuwa katika bendera za Kongo tangu ukoloni.
Bendera ya Zaire (1971-1997) |
|||
Bendera ya koloni ya "Dola huru la Kongo" (1877-1908) na baadaye Kongo ya Kibelgiji (1908-1960) |