1960
From Wikipedia
[edit] Matukio
- Januari - Hali ya dharura inakwisha katika koloni ya Kenya - vita ya Mau Mau inatangazwa imemalizika
- Januari 1 - Uhuru wa Kamerun
- Januari 9 - Ujenzi wa Lambo la Aswan inaanza nchini Misri
- Januari 23 - Jacques Piccard na Don Walsh wakitumia nyambizi ya kisayansi ya USS Trieste wanatelemka hadi kina cha (10,750 mita) chini ya UB katika Pasifiki
- Februari 1 - (Greensboro, N.C. (USA)) Wanafunzi wanne weusi wa Chuo cha Kilimo cha North Carolina wanapinga kutopewa huduma katika hoteli ya Woolworth's wakiketi chini na kukataa kuondoka. Hii ni mwanzo wa mateto mengine dhidi ya ubaguzi wa rangi katika majimbo ya kusini ya Marekani. Baada ya miezi sita wanafunzi walewale wanapokea chakula katika hoteli ile ya Woolworth's.
- Februari 13 - Bomu ya nyuklia: Mlipuko wa bomu ya nyuklia ya kwanza ya Ufaransa.
- Februari 29 - Mtetemeko wa ardhi inaharibu mji wa Agadir nchini Moroko, watu 10,000 - 15,000 wanakufa.
- Aprili 4 - Senegal inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Aprili 27 - Togo inapata uhuru Ufaransa
- Juni 26 - Madagaska inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Juni 26 - Somalia ya Kiingereza inapata uhuru kutoka Uingereza
- Juni 30 - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inapata uhuru kutoka Ubelgiji
- Julai 1 - Somalia ya Kusini inapata uhuru kutoka Italia
- Agosti 1 - Benin inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 3 - Niger - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 5 - Burkina Faso (kwa jina la Volta ya Juu) - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 7 - Côte d'Ivoire - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 11 - Chad - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 13 - Central African Republic - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 15 - Jamhuri ya Kongo - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Agosti 16 - Cyprus - inapata uhuru kutoka Uingereza
- Agosti 17 - Gabon - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Septemba 22 - Mali - inapata uhuru kutoka Ufaransa
- Oktoba 1 - Nigeria - inapata uhuru kutoka Uingereza
- Novemba 28 - Mauritania - inapata uhuru kutoka Ufaransa
[edit] Waliozaliwa
[edit] Waliofariki
- 4 Januari - Albert Camus (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka wa 1957)
- 24 Aprili - Max von Laue (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia mwaka wa 1914)
- 30 Mei - Boris Pasternak (mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi, mwaka wa 1958)