Charlotte Amalie
From Wikipedia
Charlotte Amalie ni mji mwenye wakazi 19,000 kwenye kisiwa cha Saint Thomas na mji mkuu wa Visiwa vya Virgin vya Marekani. Hii ni funguvisiwa ambayo ni sehemu ya Antili Ndogo katika Bahari ya Karibi karibu na Puerto Rico.
Mji ulipewa jina lake kutoka kwa Charlotte Amalie (1650-1714), aliyekuwa mke wa mfalme Christian V wa Denmark. Wakati ule visiwa vilikuwa koloni ya Denmark.