Frans Eemil Sillanpää
From Wikipedia
Frans Eemil Sillanpää (16 Septemba, 1888 – 3 Juni, 1964) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Finland. Anajulikana hasa kwa riwaya zake, k.m. "Urithi Duni" (kwa Kifinland Hurskas kurjuus, iliyotolewa mwaka wa 1919) au "Usingizi wa Ujanani" (Nuorena nukkunut, 1931). Mwaka wa 1939 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi.