Inchi
From Wikipedia
Inchi ni ni kipimo cha urefu wa 2.54 sentimita. Inatumika pamoja na futi na maili. Si kipimo sanifu cha kimataifa SI. Asili yake ni upana wa kidole gumba cha mtu.
Kifupi chake inchi ni " : futi 5 inchi 11 = 5' 11".
Kipimo cha inchi kiliingia katika Kiswahili tangu ukoloni wa Uingereza.
Kihistoria urefu wa inchi ilikuwa tofauti kati nchi na nchi. Leo hii inatumiwa zaidi Marekani lakini pia kwa uzoefu katika nchi zinazotumia sana lugha ya Kiingereza hata kama wameshahamia vipimo sanifu vya kimataifa SI.
Mafundi hutumia inchi wakipima unene wa bomba la maji au wa ubao uliokatwa.