Jibuti (mji)
From Wikipedia
Jibuti (Kiarabu جيبوتي) ni mji mkuu na mji mkubwa nchini Jibuti ikiwa na wakazi 400,000. Mji huu ulianzishwa kama bandari mwaka wa 1888 na Ufaransa, mji wenyewe iko kwenye rasi inayogawa Guba ya Aden kutoka Guba ya Tadjoura. Yenyewe iko 11°36' kaskazini, 43°10' Mashariki (11.60, 43.1667).
Mji huu ulianzishwa mwaka wa 1888, na mji wenyewe ukawa mji mkuu mwaka wa 1891, ukiandamwa na Tadjourah. Msafiri mmoja mwaandishi alieleza kwamba mji Jibuti kama mji ulionashida ya kujitambulisha, "alisema ya kwamba mji wa kudumu kwa taifa la wahamiaji, ni mji wa Kiafrika uliotengenezwa kama makao ya Kiulaya na pia kama Hong Kong wa Kifaransa kwa Bahari ya Shamu."
Mji pamoja na bandari ulianzishwa mwaka 1888. Mahali pake ina umuhimu wa kijeshi kwa sababu iko karibu na mlango wa bahari wa Bab el Mandeb ulio njia ya kuingia Bahari ya Shamu kutoka Bahari Hindi na kuelekea mfereji wa Suez.
Wakati wa ukoloni ilikuwa muhimu kwa Ufaransa kwa sababu meli zake ziliweza kupumzika hapa na kuongeza maji na makaa njiani kati ya Mediteranea na koloni za Kifaransa huko Vietnam.
Mji umepangwa na Wafaransa na sehemu kwa ajili ya maafisa Wafaransa upande mmoja na sehemu nyingine ya makazi kwa ajili ya Waafrika. Kaskazini mashariki kuna bandari inayotumika kwa biashara za kimataifa, uvuvi wa samaki na feri inayoenda Obock na Tadjoura.
Hulka za Mji wa jibuti ni mapwa kwa pwani ya magharibi na soko kubwa la kati, na uwanjawa mikchezo wa taifa, Jumba ya Rais na Msikiti Hamouli.
Gari la moshi laenda hadi Addis Ababa, na pia mji huu, watua ndege hushukia Kiwanja cha Ndege cha Jibuti-Ambouli
[edit] Viungo via nnje
- ll=11.558304,43.145714&spn=0.166014,0.234180&t=k&hl=en Satellite picture by Google Maps(ramani na picha za makala ya google (kiswa* g/u/g/u/l)