Kairo
From Wikipedia
Kairo (Kar القاهرة al-Qāhira – „mwenye ushindi“) ni mji mkuu wa Misri na mji mkuu wa nchi zote za kiarabu.
Kairo inakadiriwa kuwa na wakazi 7,734,614 mjini penyewe pamoja na mitaa ya karibu ni 15,502,478.
Ndani ya eneo la Kairo ya leo ulikuwepo mji wa Kiroma wa Babiloni ya Misri. Waarabu walipovamia Misri mwaka 641 walijenga karibu kambi la jeshi lao lililoitwa Fustat. Fustat ikawa makao makuu ya watawala Waislamu Misri; miji yote miwili ya Babiloni na Fustat zikakua kuwa mji mmoja ulioitwa al-Qāhira (=mji wa ushindi) au Kairo.
Piramidi za Giza ziko karibu na Kairo.
Makala hiyo kuhusu "Kairo" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Kairo kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Miji Mikuu Afrika | Misri | Miji ya Misri | Kairo | Mbegu