Kanuni ya Heisenberg ya Utovu wa Hakika
From Wikipedia
Kanuni ya Heisenberg ya Utovu wa Hakika (au Kanuni ya Utovu wa Hakika kwa kifupi) ni kanuni muhimu katika fizikia ya kwanta. Inasema kwamba haiwezekani kupima sifa mbili zinazotegemeana za kipande kimoja cha elementi kwa uhakika kabisa. Baadhi ya sifa hizo kuna mahali na mwendo. Maana yake kwa mfano, haiwezekani kupima kabisa mahali na mwendo wa elektroni moja wakati huohuo. Kanuni hii ilivumbuliwa na Werner Heisenberg mwaka wa 1927.