Keremkerem
From Wikipedia
Keremkerem | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Kerem kidari-marungi
|
||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Keremkerem ni ndege wa familia Meropidae. Wana rangi maridadi na mwili wao ni mwembamba. Domo lao ni refu na jembamba na mkia wa aina nyingi ya keremkerem una mileli mirefu katikati.
Ndege hawa wanaishi uwandani kwa kanda ya tropiki na nusu-tropiki ya Afrika, Ulaya na Asia. Hula wadudu, na nyuki, manyigu na mabunzi hasa, ambao wanakamatwa hewani. Kabla ya kula, ndege anatoa mshale wa mdudu akimgongia tawi la mti au kitu kigumu kingine.
Keremkerem hupenda kuwa pamoja kwa makundi. Huchimba mashimo ndani ya kando za mchanga kwa kutaga mayai yao meupe.
Familia ya Meropidae imegawika familia ndogo mbili: Nyctyornithinae (keremkerem wenye ndevu) na Meropinae (keremkerem wa kawaida).
[edit] Spishi za Afrika
- Merops albicollis, Kerem Koo-jeupe (White-throated Bee-eater)
- Merops apiaster, Kerem wa Ulaya (European Bee-eater)
- Merops boehmi, Kerem wa Böhm (Böhm's Bee-eater)
- Merops breweri, Kerem Kichwa-cheusi (Black-headed Bee-eater)
- Merops bulocki, Kerem Koo-jekundu (Red-throated Bee-eater)
- Merops bullockoides, Kerem Paji-jeupe (White-fronted Bee-eater)
- Merops gularis, Kerem Mweusi (Black Bee-eater)
- Merops hirundineus, Keremberere (Swallow-tailed Bee-eater)
- Merops malimbicus, Kerem Kidari-chekundu (Rosy Bee-eater)
- Merops muelleri, Kerem Kichwa-buluu (Blue-headed Bee-eater)
- Merops nubicus, Kondekonde Kaskazi (Northern Carmine Bee-eater)
- Merops nubicoides, Kondekonde Kusi (Southern Carmine Bee-eater)
- Merops oreobates, Kerem Kidari-marungi (Cinnamon-chested Bee-eater)
- Merops orientalis, Kerem Kijani (Little Green Bee-eater)
- Merops persicus, Kerem Shavu-buluu (Blue-cheeked Bee-eater)
- Merops pusillus, Kerem Mdogo (Little Bee-eater)
- Merops revoilii, Kerem Somali (Somali Bee-eater)
- Merops superciliosus, Kerem Kiole (Madagascar Bee-eater)
- Merops variegatus, Kerem Kidari-buluu (Blue-breasted Bee-eater)
[edit] Spishi za Asia
- Meropogon forsteni (Purple-bearded Bee-eater)
- Merops leschenaulti (Chestnut-headed Bee-eater)
- Merops ornatus (Rainbow Bee-eater)
- Merops philippinus (Blue-tailed Bee-eater)
- Merops viridis (Blue-throated Bee-eater)
- Nyctyornis amictus (Red-bearded Bee-eater)
- Nyctyornis athertoni (Blue-bearded Bee-eater)