Kismayu
From Wikipedia
Kismayu (pia: Kismayo au (Kisomali: Kismaayo) ni mji katika eneo la Jubbada Hoose la Somalia mwambaoni wa Bahari Hindi. Iko karibu na mdomo wa mto wa Juba.
[edit] Historia
Mji ulianzishwa na Wabajuni waliokuwa Waswahili Wabantu. Wasomali wenyewe walichelewa kufika eneo hili.
Kismayu pamoja na pwani ilikuwa chini ya masultani wa Zanzibar tangu 1835 BK. Kati ya 1875 hadi 1876 Kismayu ilitawaliwa na Misri.
Tangu 1895 ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza pamoja na Kenya lakini 1924 ilikabidhiwa kwa utawala wa Italia. Ikawa mji mkuu wa jimbo la Oltro Giuba (ng'ambo ya Juba).
Kismayu iliharibika sana kutokana na mapigano katika vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Somalia tangu 1991.