Italia
From Wikipedia
|
|||
Lugha rasmi | Kiitalia; kijimbo pia Kijerumani, Kifaransa, Kiladino, Kislovenia, Kisardinia | ||
Mji Mkuu | Roma | ||
Rais | Giorgio Napolitano | ||
Waziri Mkuu | Romano Prodi | ||
Eneo | 301.336 km² | ||
Wakazi | 58.679.441 (2005) | ||
Wakazi kwa km² | 193 | ||
JPT | 25.593 US-$ (2004) | ||
Pesa | Euro | ||
Wakati | UTC+1 | ||
Wimbo la Taifa | Fratelli d'Italia (Ndugu Waitalia) | ||
Sikukuu ya Jamhuri | 2. Juni | ||
Sikukuu ya Taifa | 25. Aprili | ||
Simu ya kimataifa | +39 | ||
Italia ni nchi ya Ulaya Kusini. Umbo lake linafanana na mguu linalozungukwa na maji ya Mediteraneo pande tatu. Imepakana na Ufaransa, Uswisi, Austria na Slovenia. Nchi mbili ndogo ndani ya eneo la Italia ni San Marino na Dola la Vatikano. Visiwa viwili vikubwa vya Sicilia na Sardinia ni sehemu za Italia pamoja na visiwa vidogovidogo. Eneo la nchi ni 301.336 km² kuna wakazi 58.679.441 (2005). Italia ni nchi iliyoendelea ikiwa na nafasi ya sita ya nguvu ya kiuchumi duniani kufuatana na JPT yake. Ni kati ya nchi sita zilizoanzisha Umoja wa Ulaya mwaka 1957.
Pia ni nchi yenye mahali pengi (40) pa kihistoria palipoingizwa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia".
Makala hiyo kuhusu "Italia" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Italia kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Nchi za Umoja wa Ulaya | ||||
---|---|---|---|---|
Austria | Cyprus | Denmark | Estonia | Finland | Hungaria | Ireland | Italia | Latvia | Lithuania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Hispania | Sweden | Ubelgiji | Uceki | Ufaransa | Ugiriki | Uholanzi | Uingereza| Ujerumani | Ureno Nchi zinazoandaa uanachama: Bulgaria | Romania
|