Korongo (Gruidae)
From Wikipedia
Korongo | ||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
![]() Korongo-taji
|
||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||
|
Makorongo hawa ni ndege wa familia Gruidae wenye domo fupi na jembamba kuliko lile la makorongo wa familia Ciconiidae. Spishi nyingi hufanya mikogo ya kubembeleza jike wakitoa sauti kubwa. Huugana kwa maishi yao yote. Spishi za nchi za halijoto wastani huhama kila mwaka kabla ya wakati wa baridi. Makorongo hawa hupenda kuwa pamoja na huhama kwa makundi makubwa. Hula kila kitu kinachopatikana, kama panya, watambaazi, amfibia au samaki, hata nafaka na matunda madogo. Spishi za makorongo zinatokea mabara yote ghairi ya Marekani ya Kusini.
[edit] Spishi za Afrika
- Grus grus, Korongo Paji-jeusi (Eurasian or Common Crane)
- Bugeranus carunculatus, Korongo Ndevu (Wattled Crane)
- Anthropoides paradisea, Korongo Buluu (Blue Crane)
- Anthropoides virgo, Korongo Tumbo-jeusi (Demoiselle Crane)
- Balearica pavonina, Korongo-taji Mweusi (Black Crowned Crane)
- Balearica regulorum, Korongo-taji (Grey Crowned Crane)
[edit] Spishi za mabara mengine
- Grus americana (Whooping Crane)
- Grus antigone (Sarus Crane)
- Grus canadensis (Sandhill Crane)
- Grus japonensis (Red-crowned Crane)
- Grus leucogeranus (Siberian Crane)
- Grus monacha (Hooded Crane)
- Grus nigricollis (Black-necked Crane)
- Grus rubicunda (Brolga)
- Grus vipio (White-naped Crane)