Maumau
From Wikipedia
Maumau ni kundi la wapiganaji wa Kenya waliokuwa wakipinga utawala wa kikoloni wa Waingereza toka mwaka 1952 hadi 1960. Ingawa vuguvugu la Maumau halikuwa na mafanikio makubwa kijeshi, upinzani wao ulichangia sana katika kuharakisha upatikanaji wa uhuru wa Kenya mwaka 1963.
Chanzo cha jina la kundi hili, Maumau, hakieleweki vyema. Kuna hali ya kutokukubaliana juu ya chanzo na maana ya jina lenyewe. Baadhi wanadai kuwa ni jina la vilima fulani huko Kenya, wengine wanaamini kuwa jina hilo lilitoka kwa masetla wa Kiingereza lililokuwa na nia ya kudhalilisha kundi hilo. Wako wanaosema kuwa jina hilo ni kifupi cha: Mzungu Aende Ulaya, Mwafrika Apate Uhuru.
Sehemu kubwa ya kundi la Maumau iliundwa na watu wa kabila la Gikuyu huku kukiwa na baadhi ya wanachama toka Embu na Meru. Wagikuyu wenyewe hawakuwa wakiliita kundi hili Maumau bali "Muingi" (vuguvugu), "Muigwithania" (anayeunganisha), "Muma wa Uiguano" (kiapo cha umoja) au KCA (Kenya Central Association, chama ambacho kilichangia kuundwa kwa kundi hili.
Makala hiyo kuhusu "Maumau" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Maumau kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Mbegu | Kenya