Max Theiler
From Wikipedia
Max Theiler (30 Januari, 1899 – 11 Agosti, 1972) alikuwa mwanabiolojia kutoka nchi ya Afrika Kusini. Baadaye alihamia na kupata uraia wa Marekani. Hasa alichunguza virusi visababishavyo maradhi mbalimbali. Pia aligundua dawa ya chanjo dhidi ya homa ya manjano. Mwaka wa 1951 alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.