Mwezi (wakati)
From Wikipedia
Mwezi ni mojawapo wa vipindi kumi na mbili vya mwaka. Muda wa mwezi unategemea na aina ya kalenda inayotumika.
Contents |
[edit] Kalenda ya mwezi
Katika kalenda ya mwezi ni sawa na kipindi kutoka awamu ya mwezi mpya angani hadi mwezi mpya unaofuata ni 29.53 siku. Mwezi mpya unaanza sawa na kuonekana kwa mwezi mpya jinsi ilivyo katika kalenda ya Kiislamu.
[edit] Kalenda ya jua
Kwa kalenda ya jua muda wa mwezi unakaribia tu muda kati ya awamu za mwezi. Katika kalenda ya Gregori miezi ina kati ya siku 28 hadi 31. Lakini vipindi hivi havina uhusiano tena na hali halisi ya awamu za mwezi wa angani mwenyewe. "Mwezi" ni lugha tu haimaanishi gimba la angani tena.
[edit] Majina ya miezi
Kwa Kiswahili miezi inatofautiana kwa namba; mwezi wa kwanza, wa pili, wa tatu ... hadi mwezi wa kumi na mbili.
Pamoja na njia kuna majina ya Kilatini iliyofika kwenye Kiswahili kupitia lugha za wakoloni yaani Kijerumani na Kiingereza.
[edit] Majina ya miezi ya asili ya Kilatini
(majina ya kilatini kamili katika mabano)
- Januari (Ianuarius), siku 31
- Februari (Februarius), siku 28*
- Machi (Martius), siku 31
- Aprili (Aprilis), siku 30
- Mei (Maius), siku 31
- Juni (Iunius), siku 30
- Julai (Iulius), siku 31,
- Agosti (Augustus), siku 31
- Septemba (September), siku 30
- Oktoba (October), siku 31
- Novemba (November), siku 30
- Disemba (December), siku 31
- Februari huongezeka siku moja kufikia 29 katika miaka mirefu kufuatana na utaratibu wa kalenda ya Gregori.
[edit] Majina ya Kiarabu ya miezi (Kalenda ya Kiislamu)
- Muharram محرّم
- Safar صفر
- Rabi`-ul-Awwal (Rabi' I) ربيع الأول
- Rabi`-ul-Akhir (Rabi' II) ربيع الآخر أو ربيع الثاني
- Jumaada-ul-Awwal (Jumaada I) جمادى الأول
- Jumaada-ul-Akhir (Jumaada II) (Jumaada II) جمادى الآخر أو جمادى الثاني
- Rajab رجب
- Shaaaban شعبان
- Ramadan رمضان
- Shawwal شوّال
- Dhul Qaadah ذو القعدة
- Dhul Hijjah ذو الحجة
Miezi hii haina wakati maalumu katika kalenda ya jua yenye miezi Januari - Desemba inabadilika kila mwaka.