Nakamikado
From Wikipedia
Nakamikado (1702 – 1737) alikuwa mfalme mkuu wa 114 (Tenno) wa Japani. Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Yasuhito. Mwaka wa 1709 alimfuata baba yake, Higashiyama, na kuwa mfalme hadi kujiuzulu mwaka wa 1735. Aliyemfuata ni mwana wake, Sakuramachi.