Nazi (tunda)
From Wikipedia

Nazi ni tunda la mbegu wa mnazi. Ina ganda la nje, ganda ngumu au mfuu wa ndani, nyama ya mbegu na utomvo ndani ya uwazi wa mbegu.
Ina matumizi mengi ya kibinadamu.
[edit] Nyama ya mbegu
- Nyama ya mbegu wake yake huliwa bichi.
- Nyama iliyokauka huitwa nguta (au: mbata). Nguta hutumiwa kwa kutengeneza mafuta ya kulika.
[edit] Ganda la mbegu
- Ganda la nje ni ya nyuzi nyingi. Zinatumiwa kwa kutengeneza mikeka, kamba na vitu vingi vingine.
- Ganda la ndani ni ngumu. Hutumiwa nyumbani kama chombo cha kikombe au cha kukorogea chakula. Kutokana na mlio wake likipigwa inatumika kama chombo cha muziki. Hutumiwa pia kama kuni. Inavaa vilevile kwa kutengeneza makaa.
[edit] Utomvu
- Utomvu ndani ya mbegu ni kinywaji safi na cha afya.
- Utomvu ukichachuka ni pombe nyepesi inayoitwa "mnazi"
- Utomvu ni safi kabisa wakati mbegu unafunguliwa hivyo unaweza kusaidia kuongeza damu mwilini mwa mwanadamu kama dawa lenyewe halipo.