Mnazi (kinywaji)
From Wikipedia
Mnazi ni pombe inayotengenezwa na utomvu wa nazi changa iliyogemwa ikiwa mtini. Utomvu huu ukikusanywa ndio unaotoa pombe ya mnazi.
Pombe hii ya mnazi ni maarufu sana maeneo ya mwambao wa pwani Tanzania ambapo minazi huota kwa wingi hasa Tanga. Pombe hii haiongezwi kitu chote ili kukamilika. Huhitaji masaa 8 tu toka kugemwa ili kukamilika kunywewa, ina rangi nyeupe iliyofifia. Mnazi ni pombe ya asili ya Wabondei toka mkoani Tanga. Pombe hii hunywewa pia sehemu nyingine ambapo minazi hukua Afrika, Visiwa vya Karibiani, Asia lakini ikiitwa majina mengine.