Paul Ehrlich
From Wikipedia
Paul Ehrlich (14 Machi, 1854 – 20 Agosti, 1915) alikuwa daktari na mwanakemia kutoka nchi ya Ujerumani. Pamoja na Sahachiro Hata aligundua dawa ya kutibu kaswende. Mwaka wa 1908, pamoja na Ilya Mechnikov alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Tiba.