Philip Anderson
From Wikipedia
Philip Warren Anderson (amezaliwa 13 Desemba, 1923) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Marekani. Hasa alichunguza upitishaji wa umeme, na usumaku. Mwaka wa 1977, pamoja na John Van Vleck na Nevill Mott alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia. Pia alikuwa stadi wa mchezo wa Kijapani Go.