Rais
From Wikipedia
Rais (kutoka kar.:رئیس) ni cheo cha mkuu wa nchi katika serikali ya jamhuri. Rais huwa anachaguliwa ama na wananchi wote au na bunge.
Kuna aina mbili za rais kufuatana na katiba za nchi mbalimbali:
- rais kama mkuu wa serikali jinsi ilivyo Marekani na pia katika nchi nyingi za Afrika (serikali ya kiraisi).
- rais kama mkuu wa nchi asiyeshughulika mambo ya serikali jinsi ilivyo Ujerumani au Uhindi (serikali ya kibunge)
Katika muundo wa serikali ya kibunge shughuli za serikali zinasimamiwa na waziri mkuu. Madaraka ya rais katika muundo huu hufanana na madaraka ya mfalme wa kikatiba isipokuwa hayupo kama rais kwa muda wa maisha yake kama mfalme.
Katika Uswisi kazi ya rais hazitekelezwi na mtu mmoja bali na Halmashauri ya Shirikisho kwa ujumla.
Makala hiyo kuhusu "Rais" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Rais kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |
Categories: Cheo | Siasa | Mbegu