Afrika
From Wikipedia
Afrika ni bara kubwa la pili duniani. Bara hili lina eneo la kilometa za mraba 30,244,050 na zaidi ya wakazi milioni 800. Asia ndio bara pekee kubwa kushinda Afrika.
Contents |
[edit] Jina la Afrika
Neno "Afrika" limepatikana kutokana na lugha ya Kilatini ya Waroma wa Kale. Waroma hawakumaanisha bara lote kwa jina hili bali eneo katika Tunisia ya leo tu. Asili yake ni katika kabila au taifa la "Afrig" walioishi sehemu zile.
Wakati huu Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini ya Bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara. Jina la "Afrika" limekuwa kawaida kuanzia karne ya 16. BK.
[edit] Lugha
tazama makala "Lugha za Afrika"
Zaidi ya lugha elfu ya Kiafrika zinazungumzwa katika Afrika leo. Lugha za Ulaya zinazumgumzwa pia, haswa Kiingereza, Kifaransa na Kireno. Kiafrikaans ni lugha ya pekee ya Afrika Kusini yenye asili ya Ulaya. Lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili) ni lugha muhimu katika Afrika ya Kusini, Afrika ya Kati na Afrika ya Mashariki. Kiarabu ni lugha muhimu Afrika ya Kaskazini.
[edit] Nchi za Afrika
Tazama makala ya pekee "Orodha ya nchi za Afrika
[edit] Vitabu
- Maria Petringa. Brazza, A Life for Africa, 2006. ISBN 9781-4259-11980.
Categories: Afrika | Bara