Ruvuma (mto)
From Wikipedia
Mto wa Ruvuma | |
---|---|
Chanzo | Karibu na Songea kwa 10° 45' kus., 35° 40' mash. |
Mdomo | Bahari ya Hindi, kusini ya Mtwara |
Nchi | Tanzania, Msumbiji |
Urefu | 1,083 km |
Kimo cha chanzo | 1850 m |
Mkondo | ?? m³/s |
Eneo la beseni | 165,760 km² |
Ruvuma (pia: Rovuma) ni mto mrefu wa Tanzania. Chanzo chake iko mashariki ya Songea katika milima ya Matagoro upande wa mashariki wa Ziwa la Nyasa. Inaelekea magharibi kati ya vilima kwenye kimo cha 1000 m karibu na Songea inageukia kusini. Mdomo uko Bahari ya Hindi kati ya Mtwara (Tanzania) na Rasi ya Delgado (Msumbiji).
Mpaka kati ya Tanzania na Msumbiji inafuata mwendo wake kwa km 730.
Tawimito muhimu ni Muhuwesi na Lumesule upande wa Tanzania halafu Lucheringo na Lujenda upande wa Msumbiji.
Inaelekea magharibi kati ya vilima kwenye kimo cha 1000 m halafu inabadilika mwelekeo kwenda kusini; inapofika mpaka wa Tanzania na Msumbiji takriban 200 km baada ya chanzo inageuka tena kuelekea mashariki hadi bahari. 35 km baada ya kuungana na Lujenda pana maporomoko ya Upinde. 160 km kabla ya kufika mdomoni bonde la Ruvuma inapanuka kuwa na upana wa 10 km; lalio la mto ni karibu mita 500 likiwa na visiwa vya mchanga. Wakati wa ukama maji hupungua sana hadi watu kuvuka mto kwa miguu; wakati wa mvua umbali kati pande zote mbili unafikia zaidi ya kilomita moja.
Mdomo mwenyewe una umbo la delta. Athira ya maji kujaa au kupwa baharini huonekana 20 km kabla ya mdomo mwenyewe. Kabla kufika kwenye delta kuna feri inayobeba magari kati ya Tanzania na Msumbiji. Feri ilipelekwa hapa na mapadre Wabenedikto wanaofanya kazi pande zote mbili za mto.
[edit] Viungo vya nje
de: "Rowuma" - Deutsches Koloniallexikon (Kamusi ya koloni za Ujerumani 1914) [[1]]