Selous
From Wikipedia
Hifadhi ya Selous ni hifadhi kubwa kuliko zote nchini Tanzania, pia ni kati ya hifadhi kubwa kabisa ya wanyama duniani.
Eneo lake ni ya 54,600 km² katika mikoa ya Pwani, Morogoro, Lindi, Mtwara na Ruvuma. Eneo hili ni kubwa kushinda nchi 70 duniani.
Tangu 1982 imeingizwa katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.
Jina limetokana na Mwingereza Ferederick Selous aliyekuwa mwindaji wakati wa kuanzishwa kwa ukoloni katika Afrika ya Kusini na Mashariki aliyeuawa Tanzania akiwa mwanajeshi wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia .
Sehemu kubwa ya eneo iko katika hali ya kiasili bili kuvurugika na shughuli za kibindadamu. Kuna tembo, kifaru, simba, twiga, kiboko na mamba.
[edit] Viungo vya nje
- en: Ukurasa wa UNESCO]