Mkoa wa Ruvuma
From Wikipedia
Mkoa wa Ruvuma ni kati ya mikoa 26 ya Tanzania.
Umepewa jina kutokana na mto Ruvuma ambao ni mpaka wake wa kusini na Msumbiji. Umepakana na Ziwa la Nyasa na Mkoa wa Morogoro upande wa magharibi, mikoa ya Iringa na Lindi upande wa kaskazini na Mkoa wa Mtwara upande wa Mashariki.
Kuna mikoa mitano ambayo ni (idadi ya wakazi katika mabano) Songea Mjini (131,336), Songea Vijijini (147,924), Tunduru (247,976), Mbinga (404,799), Namtumbo (185,131). Makao makuu ya mkoa ndipo Songea. Jumla ya wakazi wote katika Mkoa wa Ruvuma ni 1,117,166 (sensa 2002).
Makabila makubwa katika Ruvuma ni Wayao, Wangoni, Wamatengo, Wandendeule na Wandengereko.
Karibu na Songea iko monasteri kubwa ya Peramiho ya watawa Wabenedikto.
Sehemu ya mashariki ya mkoa kuna barabara ya lami kutoka Dar es Salaam kupitia Makambako na Njombe hadi Songea. Barabara kuu kwenda Lindi ni katika hali mbaya.
[edit] Viungo vya nje
- (en) Matokeo ya sensa 2002: Ruvuma Region Homepage for the 2002 Tanzania National Census
- Tanzanian Government Directory Database
- (en) Makabila ya Tanzania
|
|
---|---|
Arusha | Dar es Salaam | Dodoma | Iringa | Kagera | Kigoma | Kilimanjaro | Lindi | Manyara | Mara | Mbeya | Morogoro | Mtwara | Mwanza | Pemba Kaskazini | Pemba Kusini | Pwani | Rukwa | Ruvuma | Shinyanga | Singida | Tabora | Tanga | Unguja Kaskazini | Unguja Kusini | Unguja Mjini Magharibi | |