Shirikisho la Afrika ya Kati
From Wikipedia
Shirikisho la Afrika ya Kati iliitwa pia Shirikisho la Rhodesia na Unyasa ikiwa dola la kujitawala chini ya muundo wa ukoloniwa Kiingereza lililounganisha nchi za leo za Zambia, Zimbabwe na Malawi zilizoitwa wakati ule Rhodesia ya Kaskazini, Rhodesia ya Kusini na Unyasa (Nyassaland). Ilipatikana kati ya 1953 hadi mwisho wa 1963.
Shirikisho lilianzishwa 1. 08. 1953 kwa shabaha ya kuunda nchi itakayofuata njia kati ya muundo wa ubaguzi wa rangi ya Afrika Kusini upande mmoja na nchi huru zilizotawaliwa na wanasiasa Waafrika wenye mwelekeo wa Ujamaa. Ilikuwa jaribio la kutunza kipaumbele wa walowezi wa asili ya Ulaya.
Mwisho ulikaribia baada ya miendo ya kumaliza ukoloni duniani kote na nguvu ya wawakilishi wa Waafrika katika eneo la shirikisho iliongezeka nguvu. Mwisho wa 1963 Rhodesia ya Kaskazini ilikua taifa jipya la Zambia na Uyasa (Nyassaland) ikawa Malawi. Rhodesia ya Kaskazini ilibaki peke yake ikitangaza uhuru wake miaka kadhaa baadaye na baada ya vita ya ukombozi kuwa nchi ya Zimbabwe.