Standard Swahili-English Dictionary
From Wikipedia
Madan-Johnson's Standard Swahili-English Dictionary (kifupi: M-J SSE) iliandaliwa na wataalamu wa "Inter-territorial Language (Swahili) committee to the East African Dependencies" baada ya Vita Kuu ya Kwanza kwa ajili ya maeneo chini ya utawala wa Uingereza katika Afrika ya Mashariki. Kamati iliandaa kamusi mbili za Kiingereza-Kiswahili (M-J SES) na pia Kiswahili-Kiingereza.
Mhariri Mkuu wa kamati alikuwa katibu yake Frederick Johnson. Msingi wa kamusi hizi ulikuwa kazi ya A. C. Madan. Hivyo kamusi hizi hutajwa kama "Madan-Johnson".
Mara nyingi lugha ya kamusi hizi si tena Kiswahili cha kisasa. Lakini zimeendelea kuchapishwa mara nyingi hadi wakati wa kisasa.
Sifa ya kamusi hii ni maelezo mazuri ya asili ya maneno hasa ya maneno yenye asili katika lugha za Kiarabu, Kiajemi na lugha mbalimbali za Kibantu.
[edit] Marejeo
- Madan-Johnson, A Standard Swahili-English Dictionary (hutolewa na Oxford University Press, Nairobi & Dar es Salaam, 1939 na kuchapishwa upya mara nyingi)