Kiajemi
From Wikipedia
Kiajemi au Farsi (فارسی) ni lugha ya kitaifa ya Uajemi. Ni kati ya lugha za Kihindi-Kiajemi za lugha za Kihindi-kiulaya. Inatumiwa hasa katika nchi zifuatazo:
- Uajemi
- Tajikistan
- Afghanistan
Kuna wasemaji wa lugha ya kwanza milioni 70, na takriban wasemaji wengine milioni 60 kama lugha ya pili.
- Katika Afghanistan penye wasemaji takriban milioni 15 lugha inaitwa "dari" (درى).
- Katika Tajikistani penye wasemaji milioni 15 pia lugha inaitwa "Kitajiki".
Kiajemi ilikuwa na athira kubwa juu ya lugha mbalimbali hasa Kiarabu na Kituruki.
Kutokana na uhamiaji wa karne ya 29 lugha imepatikana katika nchi nyingi za dunia. Inaandikwa kwa herufi za Kiarabu.