Abedi Amani Karume
From Wikipedia
Sheikh Abeid Amani Karume alikuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar. Alizaliwa mwaka 1905 na kufariki tarehe 7 Aprili, 1972 kwa kupigwa risasi.
Karume aliongoza mapinduzi yaliyomwangusha Sultani aliyekuwa akitawala Zanzibar hapo mwaka 1964. Baada ya miezi mitatu Zanzibar iliungana na Tanganyika iliyokuwa ikiongozwa na Mwalimu Nyerere. Baada ya muungano wa nchi hizi mbili uliozaa jina la Tanzania, Karume alikuwa makamu wa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amani Abeid Karume, ambaye ni mtoto wa Sheikh Karume, ndiye rais wa sasa wa Zanzibar tangu mwaka 2000.