Andorra la Vella
From Wikipedia
Andorra la Vella (Kikatalani: Andorra ya Kizee) ni mji mkuu pia mji mkubwa nchini Andorra yenye wakazi 22,035.
Iko katika bonde la milima ya Pirenei kwa kimo cha m 1409. Uchumi unategemea sana utalii hasa ski miezi ya baridi.
Andorra la Vella hana uwanja wa ndege wala kituo cha treni lakini kuna huduma ya basi kwenda nje ya nchi.